STAA
wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewahi kusota lupango
ya Keko, Temeke jijini Dar es Salaam kwa miezi miwili kisa kikiwa ni
kugombea demu wa mtu. Akizungumza
na Amani juzi jijini Dar, Diamond alisema tukio hilo lilimtokea mwaka
2007 akiwa ‘andagraundi’ wa muziki wa kizazi kipya.
Diamond aliyasema hayo kufuatia kuulizwa swali na paparazi wetu kwamba, amerudiana na Miss Tanzania 2006 ambaye pi ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu. Je, haogopi kufanyiwa kitu mbaya na jamaa wake ambaye ndiye anayemuweka mjini? Msikie Diamond: Mimi simwogopi mtu eti kwa sababu natembea na demu wake. Hakuna anayeweza kunifanya lolote lile, najiamini.
“Mwaka elfu mbili na saba niligombea demu na jamaa mmoja pale Tandale (Dar). Matokeo yake jamaa akanikamata na kuniweka Gereza la Keko kwa miezi miwili, nikaachiwa baadaye, kwa hiyo sitishiki,” alisema Diamond. Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba baada ya kukamatwa alipelekwa kituo gani cha polisi na mahakama gani alipandishwa kabla ya kupelekwa mahabusu ya Keko.

Post a Comment